RAISI WA TANZANIA NA UTALII.
Mwaka 2020, ukiingia kwenye historia ya Dunia Kama mwaka mgumu sana baada ya kutokea janga la korona.
Nchi nyingi duniani zilipitia wakati mgumu kwani virusi vya korona vilikuwa havina sawa na vilikuwa vikinadilika badilika.
Hivyo uchumi wa Dunia ulishuka kwa kiwango kikubwa huku tukishuhudia sekta nyingi ziki athirika mno.
Nchi Kama Italy,Spain,Brazil,Marekani,South Africa,German, England, zili athirika vibaya sana
Hii ilipelekea kutolewa kwa sheria za kutotoka nje kwa hizi nchi na sehemu kubwa ya Dunia ilikuwa ndani yaani (Lock down)
Maisha ya wadanamu yalikuwa hatarini lakini katika nchi ya Tanzania Hali ilikuwa tofauti, RAISI wa wakati huo marehemu Dr.John Pombe Magufuli alikataza wananchi wake wasikae ndani Bali watumie mbinu za kiasili kujifukiza ili kupambana na Hali ya ugumu wa maisha na ugonjwa wenyewe.
Miaka ilisonga na Sasa baada ya kifo chake msaidizi wake makamu wa RAISI Samia Hassan Suluhu akashika hatamu.
Yametokea mengi ila baada ya kuja kwa uongozi mpya huu yeye akaja na sera ya kurudisha utalii kwa kuleta "Royal Tour" Kama sehemu ya kurudisha utalii katika Hali yake
Utalii umeanza kuzaa matunda na kurudi kwa Kasi hii ni matokeo chanya ya utalii.